Historia ya wimbo wa Ni Salama Rohoni Mwangu - Kanisani Kwanza

Historia ya wimbo wa Ni Salama Rohoni Mwangu

Share This
BWANA YESU asifiwe.
leo tunaangalia mwanzo au chanzo cha wimbo maarufu sana wa tenzi za Rohoni ambao hutumika makanisa yote ya Kikristo. yaani ''NI SALAMA MOYONI MWANGU'' au kwa jina lingine ''NIONAPO AMANI KAMA SHWARI''
Katika miaka ya 1860 Horatio aliishi na mke wake
Anna Chicago,Marekani. Spafford alikuwa
mwanasheria mkubwa aliyewekeza zaidi kwenye
majengo (real estates). Maisha yalianza kubadilika
mwaka 1870 ambapo mtoto wao pekee wa kiume
alifariki kwa ugonjwa wa nimonia, Mda mfupi baadae
janga la moto mkubwa wa Chicago uliteketeza
sehemu kubwa sana ya mali zake.
Wakiwa na matumaini ya kupunguza maumivu
waliyopata kutokana na matatizo yote,
Mwaka 1873 Spafford na mkewe walikubaliana
kwenda Uingereza ambapo rafiki yake alikuwa ana
hubiri injili.

Katika maandalizi ya mwisho kazi zilimbana Horatio,
Akawaambia mke wake na watoto wake wakike
wanne watangulie akiahidi kuwafuata haraka.
Ndipo jambo lisiloweza kufikirika likatokea, Boti
aliyopanda mke wake na watoto wake ikapata ajali
na watoto wake wote wanne walizama na kupoteza
maisha, Mke wake pekee alipona nae baada ya
kufika ufukweni akamuandikia ujumbe Spaffors ikisema
"Saved Alone, What shall I do?" yaani "Nimeokolewa
peke yangu, Nitafanya nini?"
Horatio akiwa njiani kwenda kumfariji mke wake,
akipita eneo ambalo watoto wake walizama na
kupoteza maisha ndipo aliandika mashairi ya wimbo
uliopata umaarufu sana mpaka miaka hii,
Wimbo unaitwa "it is well with my soul" / "Salama
rohoni mwangu"

Haya hapa mashairi yake kwa kiswahili na kingeleza pia.
Wimbo Na. 23 katika kitabu cha Tenzi za Rohoni.
1.Nionapo amani kama shwari, Ama nionapo shida; Kwa mambo yote umenijulisha, Ni salama rohoni mwangu.
Salama rohoni, Ni salama rohoni mwangu.
2.Ingawa shetani atanitesa, Nitajipa moyo kwani Kristo ameona unyonge wangu, Amekufa kwa roho yangu.
3.Dhambi zangu zote, wala si nusu, Zimewekwa msalabani; Wala sichukui laana yake, Ni salama rohoni mwangu.
4.Ee Bwana himiza siku ya kuja, Panda itakapolia; Utakaposhuka sitaogopa Ni salama rohoni mwangu. 

When peace, like a river, attendeth my way,
When sorrows like sea billows roll;
Whatever my lot, Thou hast taught me to say,
It is well, it is well with my soul.
(Refrain:) It is well (it is well),
with my soul (with my soul),
It is well, it is well with my soul.
Though Satan should buffet, though trials should
come,
Let this blest assurance control,
That Christ hath regarded my helpless estate,
And hath shed His own blood for my soul.
(Refrain)
My sin, oh the bliss of this glorious thoughty
My sin, not in part but the whole,
Is nailed to His cross, and I bear it no more,
Praise the Lord, praise the Lord, O my soul!
(Refrain)
For me, be it Christ, be it Christ hence to live:
If Jordan above me shall roll,
No pain shall be mine, for in death as in life
Thou wilt whisper Thy peace to my soul.
(Refrain)
And Lord haste the day, when my faith shall be sight,
The clouds be rolled back as a scroll;
The trump shall resound, and the Lord shall descend,
Even so, it is well with my soul.
(Refrain)

Baadae Anna alibarikiwa na watoto watatu, Mmoja
wa kiume ambaye alifariki akiwa na umri wa miaka
minne, na wakike wawili. Na baada ya mda walienda
kuishi Israel na familia yake wakaanzisha kundi la
kusaidia masikini huko Israel.
Binafsi Siku ya leo wimbo huu umekua ukijirudia
ndani yangu kila ninapotafakari matendo makuu
ambayo MUNGU amenifanyia hasa kwa kipindi hiki
ambacho nimezungukwa na mambo mengi, siwezi
kuwaza lolote MUNGU ni muweza wa yote.

Mwandishi; Peter M. Mabula

1 comment: