Hujafa hujaumbika, kuwa na Upendo - Kanisani Kwanza

Hujafa hujaumbika, kuwa na Upendo

Share This
Kijana mmoja alienda nje ya Nchi kutafuta maisha, akiwa huko hakuwa na uwezo wa kuwasiliana na wazazi wake kutokana na tekinolojia ya kipindi hicho kuwa duni. Lakini baada ya miaka kadhaa kupita mfomo wa tekinolojia ukawa umeboreshwa, sasa kijana akawa na uwezo wa kuwasiliana na wazazi wake kwa njia ya simu, pia akawa anawatumia pesa za matumizi pamoja na ujenzi wa nyumba ya kisasa kwani alikuwaa anajua kuwa ipo siku atarudi nyumbani kwao akiwa ameongozana na baadhi ya marafiki zake toka ughaibuni.

Hivyo wazazi wake kila wakipata pesa toka kwa kijana wao wakawa wanafanyia kazi ya ujenzi wa nyumba kama walivyoagizwa na mtoto wao, kwasababu kipindi hicho sayansi na tekinolojia ilikuwa imeshaa kuwa basi wakawa wanajitaidi sana kumtumia picha zinazo onesha kila hatua wanayoifikia hadi nyumba ilipo kamilika.

Yule kijana akawa na furaha ya kutosha kwani alikuwa hapendi wazazi wake waishi maisha duni pia aliamini sana kuwa ujenzi wa nyumba hiyo utamletea heshima kwa wageni atakao ongozana nao, baada ya mwaka mmoja kupita yule kijana akawaanda marafiki zake wawili kwaajili ya safari kisha akawajulisha wazazi wake kuwa atarudi nyumbani kusalimia akiwa ameongozana na wageni wawili. Wazazi walizipokea taarifa kwa mikono miwili huku wakiwa na shauku ya kumuona mtoto wao aliyekuwa mbali na nyuso zao kwa miaka isiyopungua 15.

Sikumoja jioni kijana akiwa anarudi toka kazini bahati mbaya alipata ajali, gari yake iligongana uso kwa uso na gari la mizigo, ajali hiyo ilipelekea kijana huyo kukatwa miguu yote  kwani ilikuwa imevunjika vibaya sana, Ooh my God!!!! yule kijana alilia sana kwani hakuwai waza kuwa iposiku angekuwa mlemavu pia akikumbuka kuwa amepata matatizo akiwa nje ya Nchi tena siku chache zikiwa zimebaki aanze safari ya kurudi kwao, basi akawa anaumia zaidi. Ikabidi safari iahilishwe na kusogezwa mbele hadi atakapo pata nguvu.

Kampuni iliyokuwa imemuajili kijana huyo ilisikitiswa na kuhuzunishwa na tukio lililo jitokeza pia waliumia kwasababu huyo kijana asingeweza kuendelea kuwa mfanya kazi wa kampuni hiyo kutokana na aina ya ulemavu alio upata. Basi wakaamua kumchangia pesa ya kutosha ili atakapokuwa kwao iweze kumsaidia kuishi kwa amani. Wakati huo huyo kijana alikuwa anahudumiwa na familia moja ya rafiki yake kwa mda wa mwaka mzima hadi alipopata ahueni, Tangu apate ajali alikuwa bado hajawajulisha wazazi wake kuwa amepatwa na matatizo hayo japo aliwajulisha kuwa safari imeahilishwa kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wake.
Basi sikumoja alianza kutafakari namna familia ya rafiki yake ilivyo ishi naye kwa upendo ukilinganisha na matatizo aliyokuwa nao, akawaza na kuona anarafiki wa pekee sana, ukizingatia hakuwa ndugu yake. Baada ya kuwaza hivyo akaamua kuwapigia wazazi wake simu ili kujua kama wanaweza ishi na mtu mlemavu.

Alianza kuongea na mama yake kwanza " Mama mwezi ujao narudi nyumbani, nitakuja kuishi hapo nyumbani na rafiki yangu, mama akaitikia kwa furaha tunawakalibisha sana mwanangu, mimi na baba yako tumekumic sana mwanangu, itabidi siku hiyo tufanye sherehe kubwa sana" Yule kijana akasema lakini mama naomba nikushilikishe kuwa rafiki yangu ni mremavu, alipata ajari hivyo hana miguu yote ila kwasababu amenisaidia sana tangu nilivyofika hapa naomba nije kuishi naye hapo nyumbani, Yule mama alibadilika akasema mwanangu hiki sii kituo cha kulelea walemavu, hizo taarifa zitaki kabisa kuzisikia, unataka utuletee mzigo? Sisi tuwe watu wa kulea mlemavu kisaa kakusaidia? Ni bora uwe masikini ila siyo huo mzigo, yule kijana akasema sawa mama nimekuelewa naomba niongee na baba,

baba yake alipopewa maelezo naye akatoa msimamo kama uliotolewa na mama yake. Basi yule kijana akawa analia kutokana na majibu aliyopewa na wazazi wake, ukizingatia yeye ndo mlemavu ila wazazi wake hawajui ndio maana wanaongea hivyo bila kujua kuwa mtoto wao ndo mhangwa, akawa amepata picha waliyonayo wazazi wake juu ya walemavu. Akajiwazia moyoni kama ile familia ya rafiki yake ingekuwa na roho kama ya wazazi wake ingekuwaje??, akaamini kuwa huenda asingekuwa hai, amaa laa angeishi maisha ya taabu sana, Mawazo yakamzidi,akaona bora kufa, kwa hasira alijitupa toka juu ya ghorofa ili afe lakini haikuwezekana.

Baadaye yule kijana alisafiri hadi kwao na kufikia hotelin, akawasiliana na baadhi ya ndugu wakaja kumuona na kumsaidia kununua nyumba atakayo ishi akiwa mbali na wazazi wake ambao walisema hawawezi kuishi na mtu mlemavu, lakini hata hivyo taarifa ziliwafikia wazazi wake ndipo sasa wakaja kujua kuwa mtoto wao ndiye aliyekuwa mlemavu na siyo rafiki yake kama walivyo ambiwa kwenye simu.Hakika wale wazazi waliumia kuona mtoto wao yupo vile huku wakiyakumbuka maneno waliyoyatoa bila kujua kuwa mtoto wao ndo mlemavu.

Hata hivyo walimuomba msamaha mtoto wao kwa moyo wa ukatili waliouonesha dhidi ya walemavu, naye akawaomba msahamu kwa kujalibu kujiua kutokana na maneno yao.

Umejifunza nini?
Jee kati yetu yupo anayeijua kesho yake?
Hujafa hujaumbika, unapokuwa mzima wa mwili usijione wewe unahaki sana ya kuwa hivyo hadi ukahisi wale walemavu walifanya uzembe furani hadi wakawa walemavu.

No comments:

Post a Comment