Mwalimu mmoja aliita wanafunzi wake akawaambia''Kesho kila mwanafunzi
aje na nyanya kulingana na idadi ya watu anaowachukia, Yaani kama
unamchukia mtu mmoja uje na nyanya moja kama ni wawili basi njoo na
nyanya mbili vilevile.
Nyanya hizo mtazibeba kwenye mabegi yenu ya kubebea madaftari na vitu vingine vya shule*
"Wanafunzi wakakubali halafu kesho yake wanafunzi wakazibeba zile
nyanya vizuri kabisa wengine walibeba moja,wengine mbili na wengine
nyingi sana.
Kama mwalimu alivyosema zile nyanya zikapewa majina ya watu ambao wanafunzi wanawachukia
Baada ya kuzipa hizo nyanya majina mwalimu, akawaambia kila
mwanafunzi azirudishie nyanya zake kwenye begi lake halafu aziache humo
humo ndani ya begi kila siku awe anakuja nazo shuleni na kurudi nazo
nyumbani.
Baada ya siku kadhaa wanafunzi wakaanza kulalamika hasa
wale waliobeba nyanya nyingi kuwa nyanya ni nzito sana na zinatoa harufu
mbaya na zinaharibu vitu vyao vizuri walivyoweka kwenye mabegi yao
Mwalimu akawaambia hivi ndivyo ilivyo mtu unapoweka watu usiowapenda moyoni
kama mtu huwezi kuvumilia kukaa na harufu ya nyanya, kwenye begi vipi
kuhusu madhara ambayo moyo wako unayapata kwa kuubebesha mzigo wa chuki
dhidi ya watu.?
Moyo unapata madhara makubwa sana unapobebeshwa
chuki kila wakati kila siku moyo unakuwa na chuki na hapo ndipo
unaharibika, na kusababisha kuharibu hata vitu vingine vizuri
vilivyokoko moyoni mwako. Moyo ni kama lile begi la kubebea madaftari
unahitaji kubeba vitu vizuri na visivyo na chuki ndani yake
Safisha moyo kwa kusamehe wanaokukosea, jifunze kusamehe maana ni moja
ya virutubisho vya moyo wako,Samehe kwa kila anayekukosea na kukukwaza
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kusamehe ni muhimu sana, lipo somo lingine kama hilo mtu akijifunza atanufaika zaidi..fuata link hii... https://wingulamashahidi.org/2018/11/20/samehe-kutoka-ndani-ya-moyo-wako/
ReplyDelete