Kama kwenda kanisani ,Kubeba Biblia ,Kusema tumeokoka,Kuwa watumishi
,Kuwa viongozi na Kuwa mkristo na kuimba ndo kuingia katika Ufalme wa
Mbinguni ,,Hahahaha Hakika Jehanamu atakwenda Shetani na maraika zake
walioasi pamoja nae mbinguni tu.
Ni wengi tunaobeba Biblia ,Ni
wengi wakristo ilihari hata huyo Krsto Yesu hawana mahusiano naye kabisa
Ni shida ,Ni wengi tunakwenda makanisani lakini hicho si kipimo cha
kututhibitishia au kutupa uhakika wa kuingia katika Ufalme wa mbinguni
,Maana hata wenye dhambi makanisani wapo wanakwenda na wengne wamezoea
kumekuwa kama nyumbani kwao kabisa wapagani hao .
Ni wengi
wanaimba makanisani N.K lakini si kipimo cha kuwathibitishia kuingia
katika Ufalme wa Mbinguni ,Maana hata wapagani wanaimba sana
wanajitafutia kipato ila Ni wapagani wakubwa watenda dhambi sana,Ni
wengi Watumishi wa Mungi lakini si wote Ni watumishi wa Mungu
,Wanajiita Ni hivyo lakini Mungu hajawatuma Ni watumishi wa uongo ,Je
nao waingie katika Ufalme wa Mbinguni hapana haiwezekani.
Ni
wengi wanaobeba Biblia lakini si wote waliookoka ,Na wengne wanasema
Kuwa wameokoka je nao waingie katika Ufalme wa Mbinguni hapana Maana
wokovu si kusema mdomoni tu hapana ,Maana wengi wanakili hivyo ila
matendo yao yapo kinyume na kauli zao ,Ni watenda dhambi wakubwa kwa
siri sana.
Na wengi ni viongozi wa Dini,Madhehebu na makanisa
je wote waingie katika Ufalme wa Mbinguni hapana ,Maana hata wenye
dhambi wanashika nyazifa mbalimbali katika makanisa,madhehebu na Dini
WOKOVU WA MDOMONI HUU HAPA
Tito>>>1::16 Wanakiri ya kwamba wanamjua Mungu ,Bali kwa
matendo yao wanamkana ni wenye machukizo ,Waasi ,wala wala kwa Tendo
jema hawafai . TRUE GOSPEL.
UTHIBITISHO WA WEWE KUINGIA HUU.
Mathayo 7:20--21 Ndipo kwa matunda yao mtawatambua.
21>>Si kila mtu aniambiaye Bwana Bwana atakayeingia katika Ufalme
wa Mbinguni, Bali Yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye Mbinguni.
YESU AMEWEKA WAZI KAZI KWETU.
Tunaingia Mbinguni kwa Kuishi,Kutenda na Kuamini sawa sawa na Neno la
Mungu au tukiyafanya mapenzi ya Mungu tu ndo tutaingia mpendwa .
Wokovu si kusema mdomoni tu kutangaza au kujielezea hapana Bali
matendo yao yatakushuhudia wazi Yale unayofanya kwa siri na kwa uwazi
kwamba utaingia Mbinguni au unawasindikiza wengne tu we we ni mpagani
aliyejivika vazi LA kondoo ila ni mtenda dhambi mzuri tu .
WARUMI
2::13 Kwa sababu si wale waisikiao Sheria walio wenye haki mbele za
Mungu ,Bali ni wale waitendao sheria watakaohesabiwa haki.Hallelujah
MTU wa Mungu wakati uliokubalika ni sasa Amua sasa Usiendelee
kusalisali ,Kuimba imba na kutumika tumika bila faida yoyote Mpokee Yesu
Leo WARUMI 10:9,10 .
NA ninyi mliokoka Tuliokoka na Waluokoka
Tujitathimini Wokovu wetu mahusiano yetu na Yesu krsto ni ya kuridhisha
au Twajidanganya wenyewe Kwa kufanya dhambi kwa siri ,,Maana Afichaye
dhambi zake hatafanikiwa Bali yeye aziungamaye na kuziacha Atapate
Rehema kwa Mungu .
SIHUKUMU TUTAFAKALI MPENDWA .
True gospel for all nations "Amen.
UMEJIANDAAJE KUINGIA KATIKA UFALME WA MUNGU ?
Mwandishi; Mch. Gody Lwanzaly
Kuingia katika Ufalme wa Mbinguni, si jambo jepesi
Share This
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment