Yeremia 23:23 “Mimi ni Mungu aliye karibu, asema BWANA, mimi si
Mungu aliye mbali.” Je! Umewahi kujiuliza kuwa, mara nyingi umekuwa
ukiomba na hauoni majibu wakati Mungu amesema kuwa YEYE ni Mungu aliye
karibu na wewe?
Kwa nini hajibu maombi yako? Unapaswa kuchunguza
mahusiano yako na YEYE yakoje, YEYE ni Mtakatifu; Je! Unaishi katika
Utakatifu? YEYE Anasamehe, Je! wewe Unasamehe wale wanaokukosea?
Mungu anataka upokee Mema kutoka kwake, hivyo JICHUNGUZE wewe mwenyewe kuwa je! Unatii sheria zake?
Je unajiuliza kwanini maombi yako hayajibiwi?
Share This
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment