Hivyo akaanza kuomba kwa Mungu amuepushie na hilo janga, kwani anajua kama angekamatwa angeuawa vibaya sana. "Mwenyezi Mungu niokoe na hiki kifo kilicho mbele yangu, na nitaishi nikikuabudu wewe"Wakati akiendelea kushangaa shangaa pale, akaona kuna mapango kadhaa chini ya ule mwamba wa mawe, hivyo akaamua kuingia ndani ya pango mojawapo. Akiwa ndani akasikia adui zake wakimtafuta pango moja baada ya jingine "atakua ameingia humu, hebu chungulieni"- alisikia wakiambizana na kama pango lilikuwa giza walililipua na bomu ili yoyote aliyemo ndani afie humo humo.
Mwanajeshi aliingiwa na wasiwasi mno maana alijua kwamba wakifika katika pango ambalo yumo, hata wakimchungulia wasipomkuta watalipua tu bomu na yeye atafia humo.
Hivyo akazidi kumuomba Mungu, "Oh Mungu wangu, niokoe na hiki kifo kibaya"- wakati akiendelea kuomba akaona buibui akitokea mbele ya lile pango kwenye ule mlango, buibui akaanza kujenga utando wake.
Askari akamuuliza Mungu, "Badala ya kuliziba pango na mawe makubwa, umetuma buibui ndio ajenge utando?? Itawezaje kuniokoa mimi? Baada ya kuona hilo askari akapoteza matumaini ya kupona na akalala tu pale kusubiri kulipuliwa.
Baada ya maadui kufika katika pango alilopo, Mwanajeshi mmoja akataka kurusha bomu ndani, ila kamanda wake akamkaripia..."wewe mpumbavu, huoni huo utando wa bui bui hapo kwenye mlango wa pango? Unataka kumaliza tu bomu zetu chache zilizobaki.
Yule askari aliyetaka kulipua akamuuliza kamanda wake, "unamaanisha nini kamanda?"
Kamanda akajibu, "ninamaanisha kwamba kama huyu mpumbavu mmoja aliyebaki angekimbilia humu basi angevunja huo utando wa bui bui, sasa buibui alivyojitanda hapo na huo utando wake huyo mtu angeingiaje bila kuuvunja? kifupi hamna mtu humo, twendeni mbele tutamkamatia huko huko, hivyo wakaondoka na kuendelea kulipua mapango yaliyofuata.
Askari akawa ameokoka na kifo.....akiwa ndani ya pango akainama na kumwambia Mungu "Nisamehe Mungu wangu kwa kudharau njia zako, asante kwa kuokoa maisha yangu"
Mpendwa,
katika siku hizi za mwisho wa dunia unaweza ukawa katika matatizo
makubwa, lakini kamwe usichoke kumuomba Mungu. Mungu anaweza kukujibu
kwa namna yake yoyote ile inaweza ikawa ndogo tofauti na wewe
ulivyofikiria. Ila usisahau kwamba utando wa buibui uliojengwa na Mungu
ni imara zaidi ya ukuta wa matofali uliojengwa na binadamu.
Imeandikwa na mwandishi mwalimu habelnoah
Share ujumbe na Mungu akafanye njia pasipo njia kuwa na njia katika maisha yako katika jina la Yesu.
Imeandikwa na mwandishi mwalimu habelnoah
Share ujumbe na Mungu akafanye njia pasipo njia kuwa na njia katika maisha yako katika jina la Yesu.
No comments:
Post a Comment