Unabii wa Yesu kuhusu hekalu la Yerusalemu-Sehemu 1 [Askofu Sylivester Gamanywa] - Kanisani Kwanza

Unabii wa Yesu kuhusu hekalu la Yerusalemu-Sehemu 1 [Askofu Sylivester Gamanywa]

Share This
“Yesu akaenda zake, akatoka hekaluni; wanafunzi wake wakamwendea ili kumwonyesha majengo ya hekalu. Naye akajibu akawaambia, hamyaoni haya yote? Amin, nawaambieni, halitasalia jiwe ambalo halitabomoshwa.” (MT.24:1-2)

Unabii wa kubomolewa kwa majengo ya Hekalu ulikwishi kutimizwa rasmi mnamo mwaka 70 B.K ambapo Warumi waliuhusuru mji wa Yerusalemu na kulibomoa hekalu zima kama Yesu alivyokwisha kutabiri.

“Basi hapo mtakapoliona chukizo la uharibifu, lile lililonenwa na nabii Danieli, limesimama katika patakatifu (asomaye na afahamu) ndipo walio katika Uyahudi na wakimbilie milimani, naye aliye juu ya dari asichuke kuvichukua vilivyomo nyumbani mwake; wala aliye shambani asirudi kuichukua nguo yake…” (MT.24:15-18)

Unabii huu unataja tena habari za “chukizo la uharibifu” kusimama “mahali patakatifu”, ukimaanisha kuwepo kwa hekalu jingine ambalo ndani yake kuna sehemu ya “mahali patakatifu”.
Aidha unabii huu unataja habari za tukio ambalo litafanyika wakati wa dhiki kuu ya siku za mwisho.
Kwa maneno mengine, hekalu linalotajwa katika unabii huu ni hekalu jipya ambalo litakuwa limejengwa jijini Yerusalemu.

Yesu asingezungumuzia hekalu lile lile la kwanza ambalo alijua litavunjwa halafu aseme habari za "chukizo la uharibifu" kusimama "mahali patakatifu" pa hekalu ambalo litakuwa limevunjwa.
Sasa basi, kama vile unabii wa Yesu wa kwanza kuhusu kuvunjwa kwa hekalu ulivyotimia mwaka wa 70 B.K; hali kadhalika ndivyo hata hivi sasa, tunatarajia kutimia kwa unabii wa pili wa kujengwa hekalu jipya ambalo litakuja kunajisiwa na "chukizo la uharibifu" kama Danieli alivyotabiri.
Jumapili hii nitawasilisha "kalenda ya kinabii" ya kutimizwa kwa unabii huu kwa mujibu wa maandiko ya Biblia.

Vuguvugu la malumbano kuhusu mji wa Yerusalemu hivi sasa ni harakati za kutimizwa unabii uliotabiriwa na Yesu mwenyewe wakati wowote kuanzia hivi sasa
Kama unaamini katika unabii wa Yesu Kristo basi nijulishe kwa ku-like post hii na wajulishe na marafiki zako pia. Karibu Jumapili hii BCIC Mbezi beach tuipitie kalenda ya kinabii.

No comments:

Post a Comment