Wakati wana wa Israeli wakiendelea na safari ya Kuelekea Kaanani tangu walipotoka Misri
Sasa walipofika kwenye mlima Sinai, Mungu alimwita Mussa afike mlimani kwa ajili ya
kumpa sheria mbalimbali wana wa Israeli wanapaswa kuanza kuzifuata. Maana kabla ya hapo walikuwa wanaishi tu bila ya sheria yoyote. Kwa kuwa wakati Musa anaondoka kwenye kusema na Mungu hakusema Kuwa
atatumia Siku ngapi, au atakaa kwa Siku ngapi atakuwa amerudi hilo hakusema
bali aliondoka...
Na Musa ndiye kiongozi mkuu wa ile safari,
isingewezekana wana wa Israeli kuondoka kuendelea na safari bila Musa
hivyo iliwalazimu kumsubiri tu Musa mpaka atakaporudi kisha waendelee na
safari ya kuelekea Kaanani
Hivyo walimsubiri Siku ya kwanza, ya pili, ya tatu, ya nne, ya tano bila Mafanikio bado Musa hakuwa amerejea, waliendelea
Kumsubiri na Kuvumilia mpaka siku ya 39 bado hakuwa amerejea kutoka mlimani. Mara baada ya kuvumilia sana mpaka kuchoshwa na uvumilivu wao na kuona hakuna haja ya kuendelea kusubiri sana, mwisho wakapata cha kuamua
KUTOKA 32:1
Hata watu walipoona ya Kuwa Musa amekawia kushuka Katika mlima,
wakakusanyana wakamwendea Haruni, wakamwambia, haya katufanyizie miungu
itakayokwenda mbele yetu kwa maana Musa huyo aliyetutoa Katika nchi ya
misri hatujui yaliyompata..
Haya
ndiyo maamuzi ambayo wana wa Israeli waliposhindwa kusubiri na Kuvumilia
mpaka Musa arudi. Lakini kuna funzo kubwa Sana ambalo Nataka
nikushirikishe ambalo linaweza kukusaidia kwa namna Moja au nyingine
Siku
ile ile ambayo walichukua uamuz wa kutengeneza ndama na kuiabudu baada
ya kuona Kuwa Musa amekawia kushuka NDIYO SIKU HIYO HIYO MUSA ALIKUWA
ANASHUKA TOKA MLIMANI. Tunaona hapa
KUTOKA 31:18
Hapo BWANA alipokuwa amekwisha zungumza na Musa Katika mlima wa Sinai,
akampa Hizo mbao mbili za ushuhuda, mbao mbili za mawe zilizoandikwa kwa
chanda cha Mungu..
Kumbe ni siku ile ile ambayo Musa alikuwa
anajiandaa Kurudi ndiyo Siku hiyo, nao wana wa Israeli walitengeneza na
kuiabudu ndama
Kumbe wangevumilia kidogo tu kile ambacho walikihitaji wangekipata, Pia
Walivumilia Siku nyingi lakini wakati Siku ya Muujiza wao umefika
wakawa wametoka nje ya mstari..
Ndivyo ilivyo wengi leo
wanavyopishana na miujiza yao kwa KUSHINDWA KUVUMILIA mpaka Siku ya
mwisho wanavumilia lakini wakati wao wa kupata miujiza yao inapokaribia
wanakuwa wameshatoka nje ya mstari.. Kwa kutengeneza ndama
Inawezekana mpendwa labda Musa wako ni ndoa umekaa muda pasipo kupata
Mchumba, labda ni kazi, fedha, sikia nikwambie Endelea kuvumilia na
kusubr mpka Musa wako ashuke mlimani usije ukaamua kutengeneza ndama,
ukasema sasa yeyote tu atakayetokea mimi huyohyo, au ukaamua kufata njia
unazozijua wewe mwenyewe
Wengi leo wanaoomba wanapishana na
miujiza yao pale wakiona kimya wanakata tamaa, lakini Siku ile
wanapokata tamaa na Kuacha kuomba kumbe hawajui Siku ya miujiza yao
imekaribia
Haijalishi ni nini umesubr kwa Mungu na kwa muda gani
hakijatokea USIACHE kuvumilia na kusubr maana hujui ni linii Muujiza
wako utafika
Imeandikwa na Mwalimu Exon Albert-0656286062
Imesahihishwa na Barnabas Gwakisa
Kuongezeka kwa usiku, ndiko kukaribia kwa asubuhi
Share This
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment